Zaburi 91:9-12
Ukisema, “BWANA ndiye kimbilio langu,” na kumfanya Aliye Juu kuwa makao yako, hakuna madhara yatakayokupata, wala maafa hayatakaribia hema yako. Kwa maana atawaamuru malaika zake wakulinde katika njia zako zote; watakuinua mikononi mwao, usije ukapiga mguu wako katika jiwe.