Mathayo 3:11-12
“Mimi nawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini baada yangu anakuja aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa [b] Roho Mtakatifu na moto. Kipepeo chake kimo mkononi mwake, naye atasafisha nafaka yake, akikusanya ngano ghalani na kuyateketeza makapi kwa moto usiozimika.”